Boma Hai FM ni redio ya jamii inayohudumia wakazi wa Wilaya ya Hai na maeneo ya jirani mkoani Kilimanjaro, Tanzania. Redio hii imeanzishwa kwa lengo la kutoa jukwaa huru la habari, elimu, burudani na mijadala ya kijamii inayogusa maisha ya kila siku ya wananchi. Kupitia vipindi vyake mbalimbali, Boma Hai FM inalenga kuelimisha jamii, kukuza mshikamano, kuhamasisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi, pamoja na kusimamia maadili na utamaduni wa Kitanzania.
Boma Hai FM inarusha matangazo kwa masafa ya 89.3 MHz na sasa pia inapatikana mtandaoni kupitia radio online, ili kuwafikia wasikilizaji waliopo ndani na nje ya nchi. Redio hii inatoa vipindi vya habari za ndani na kitaifa, vipindi vya elimu kwa jamii, vipindi vya vijana, wanawake na watoto, pamoja na burudani inayojumuisha muziki wa asili